Huduma Tunazotoa

1. Kufikia Soko na Kuunganisha Wateja.

Tuna uhusiano mzuri wa masoko ya ndani na kimataifa, na kutokana na ukweli kwamba wakulima wengi hawajaunganishwa vya kutosha na masoko haya, Tunatoa huduma ya kuwaunganisha wadau wa kilimo na masoko ya mazao yao, pia tunawaunganisha wadau wa ushirika na wadau wengine kwenye sekta nyingine za kimkakati. Tunafanya hivi kwa kutambua mahitaji ya soko na pale inapowezekana kutoa mafunzo ya kitaalam au mahususi kwenye maeneo maalum kama usalama wa chakula, usafi, matumizi salama ya dawa za kuua wadudu (viwatilifu) na huduma  baada ya mavuno na masoko.

mafunzo

2. Usimamizi wa Shamba, Vikundi vya Kijamii na Huduma za Ushauri kwa Biashara za Ushirika.

 

USIMAMIZI WA SHAMBA 

Tunatoa suluhisho kamili kwa wajasiriamali wa biashara ya kilimo, moja kwa moja kutoka kwenye ushauri wa kitaalamu kuhusu uchaguzi wa mradi, utafiti wa uzalishaji (ikiwa ni pamoja na ardhi na rasilimali asilia), uchambuzi wa gharama na faida, uandaaji wa mpango biashara na usimamizi wa jumla wa shamba.

Tuna timu ya wataalam wenye uzoefu kwenye  kilimo, wataalamu wa lishe, wahandisi wa kilimo, na mameneja wa shamba watakaosimamia uwekezaji wako kutoka kwenye maandalizi ya shamba hadi kuvuna mazao yoyote unayoyachagua.

Tunatoa huduma za kupanga shamba (farm layout) kwa mazao ya kudumu kama vile ndizi, embe, machungwa, miwa, n.k.

Pamoja na kutoa huduma za usimamizi wa mifugo. 

 

VIKUNDI VYA KIJAMII NA USHIRIKA

 Kwa kutumia Sheria za Ushirika, kanuni, miongozo, na maelekezo kutoka kwa mamlaka zilizopewa jukumu la kusimamia vya vya ushirika, tunahakikisha ufanisi na uendelevu katika usimamizi wa biashara ya ushirika kwa kutoa msaada wa kitaalam k katika kuanzisha na kusimamia biashara za ushirika.

Tunatoa pia msaada kwa vikundi vya kijamii (HBOs) katika kuhamasisha, kuanzisha, kurasimisha na kuratibu mifumo ya kiuongozi na utawala. 

Tunatoa mafunzo kuhusu:

Muktadha na Upeo wa Ushirika.

Umuhimu wa Ushirika katika Mtazamo wa Kiuchumi, Kijamii, na Kitamaduni (kwa nini kujiunga na ushirika?) .

Usimamizi na Utawala wa Ushirika.

Usimamizi na Udhibiti wa Ndani wa Ushirika.

Uratibu na Utatuzi wa migogoro.  

 

3. Mafunzo

Tunalenga mafunzo yetu kwenye mahitaji ya sasa kwakuzingatia mahitaji ya masoko ya ndani na kimataifa, mafunzo yetu yameelekezwa katika maeneo yafuatayo: Misingi ya Usafi wa Chakula, Mbinu Bora za Kilimo, Mbinu Bora za Utengenezaji, Matumizi Salama ya Dawa za Kuua Wadudu, kupanga na kusimamia  Biashara ya Kilimo, Kuvuna na Kusindika Baada ya Kuvuna, Mifumo ya Usimamizi wa Usalama wa Chakula (FSMS), Mifumo ya Usimamizi wa Mazingira (EMS), Ufuatiliaji wa Bidhaa, Uzingatiaji wa misingi na maadili ya Biashara, Usimamizi na Utawala wa Taasisi, Uanzishaji, Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Jamii, Udhibiti wa Ubora wa Taasisi, Usimamizi na Utawala wa Ushirika, Usimamizi wa biashara ya Mifugo na ufugaji, Matibabu ya Magonjwa na Udhibiti.

kilimo cha kisasa cha mahind

4. Mbinu Bora za Kilimo na Ushauri wa Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki.

 

Tuna timu ya wataalam wa kilimo na wataalam wa Usimamizi wa Mazao ya jumuishi (ICM) ambao watatembea nawewe na kukushauri juu ya njia bora ya kushughulikia usimamizi wa udongo na rutuba, mapendekezo ya mbolea, usimamizi wa wadudu na magonjwa, na mbinu za kuzalisha mimea bandia ikiwa ni pamoja na ufugaji. wataalam wetu watatembea nawe kutoa ushauri bora kwa mavuno bora na uzalishaji unaofaa kifedha. Pia tunasimamia mashamba kwa niaba ya mteja kutoka hatua ya kupanda hadi kuvuna.

Tunayo timu ya wataalam wa uzalishaji wa nyuki, usindikaji, na masoko ya bidhaa za nyuki na bidhaa nyingine zinazotokana na nyuki kama vile kutengeneza sabuni, mafuta ya kujipaka yenye harufu nzuri, varnishes, dawa ya viatu, mishumaa, na zingine nyingi kulingana na mahitaji ya mteja.

5. Uchambuzi wa Mnyororo wa Thamani

Tuna ujuzi wa kuchunguza kwa undani mnyororo wako wa thamani, kuelewa uwezo na fursa muhimu, kutambua maeneo yanayohitaji marekebisho ili kubaki na faida. Wataalam wetu wanaelewa kikamilifu kilimo na biashara za ushirika nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na changamoto zote na mambo yanayochangia gharama zinazohusiana na uwekezaji katika kilimo na biashara za ushirika.