Our Projects

Mradi wa Michikichi

Zao la michikichi ni zao linalo endelea kuwa bora na linalo kuza kipato cha kaya mbalimbali katika ukanda huu tuliopo.mpaka sasa tunazo hekari karibu ishirini katika maeneo tofauti ambazo tunaendelea kuzisimamia, pia kutoa ushauri kwa wakulima wengine wa michikichi na mazao mengine yote.

Mradi wa mpunga

Kilimo cha kisasa cha mpunga kwajili ya biashara na chakula, mpaka sasa tunasimamia mashamba mbalimbali ya wateja jumla yake ni hekari elfu moja yanapatikana maeneo tofauti tofauti kama uvinza na kaliuwa. Tunayo furaha ya kuwakaribisha wateja wapya pia.

mladi wa mahindi

Mradi wa mahindi.

Hili ni moja ya shamba la mahindi tunalosimamia kutoka hatua ya mwanzo mpaka hatua ya kuvuna. linapatikana eneo la kidiami kasulu mkoani kigoma na lina ukubwa wa hekari kumi. pia tunamashamba mengine ya mahindi katika maeneo mengine ikiwemo kagera kanda mkoani kigoma ambalo lina hekari mia moja na kibondo vijijini ambalo lina hekari nane.

Kilimo cha kisasa cha mahindi kwa kuzingatia masharti yote na uchaguzi sahihi wa mbegu, mbolea ,aina ya ukanda, kuzingatia vipimo vyote mdaa wa kupanda na mengineyo.

Mradi wa maharage

Hili ni moja ya shamba lenye ukubwa wa hekari tano na tunalisimamia kutoka hatua ya mwanzo kabsa ya uandaaji wa shamba mpaka mavuno linapatikana eneo la kidiami. ukiachana na hilo pia tunashamba lingine lenye ukubwa wa hekari kumi linalopatikana kijiji cha kibondo.

Kilimo cha kisasa cha maharage kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote ikiwemo uchaguzi wa mbegu bora, mbolea, dawa (viwatilifu) na mengineyo .

Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya mashamba tunayo simamia

CHAGUO LAKO NI JAYS & N GENERAL SUPPLIES AND CONSULT COMPANY LIMITED.

DIRECTOR